NAPLES ZOO YATOA MSAADA WA MAHEMA KUSAIDIA UHIFADHI WA FARU WEUPE NGORONGORO*


Katika kuendeleza juhudi za kuimarisha uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za Wanyamapori, Taasisi ya Caribbean Naples Zoo kutoka Nchini Marekani imetoa msaada wa mahema kumi (10) kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa lengo la  kuimarisha shughuli za uhifadhi wa Faru weupe na wanyama wengine waliopo katika eneo la urithi wa dunia la Ngorongoro.

Mwakilishi wa Caribbean Napple Zoo Tanzania  Albert Mollel ameeleza kuwa taasisi yao kusaidia vitendea kazi hivyo ni muendelezo wa ushirikiano katika kuimarisha ulinzi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za  wanyamapori hasa adimu na waliopo hatarini kutoweka kama Faru. 

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Kamishna wa Uhifadhi NCAA Bw. Abdul-Razaq Badru ameishukuru Caribbean Naples Zoo kwa msaada huo muhimu na kusisitiza kuwa vifaa hivyo vitawawezesha askari wa uhifadhi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi katika ulinzi wa Faru na wanyama wengine waliopo Hifadhi ya Ngorongoro.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO