Posts

Showing posts from November, 2025

VIJANA MTWARA WATAKA FURSA

Image
Na. OR – MV, Mtwara Vijana wa mkoa wa Mtwara wamesema wanahitaji Serikali iwasaidie kuweka mazingira wezeshi ili fursa za kiuchumi zilizopo ziwasaidie kuzalisha ajira na kudumisha amani ikiwa ni matunda ya kuanzishwa wizara ya vijana kwa mara ya kwanza nchini. Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati na vijana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana na mbunge wa Mtwara Mjini Joel Nanauka (29 Novemba 2025) mjini Mtwara alisema Serikali itatumia muda mwingi kutafuta fursa za maendeleo kwa vijana badala ya kudhibiti vijana. Waziri wa Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka aliwaeleza vijana kuwa dhmaira ya kuundwa wizara hiyo ni kutekeleza maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuona mawazo na fikra za vijana nchini zinasikika ili kutatua changamoto zao. Nanauka aliongeza kusema katika kuhakikisha vijana wanapata mitaji na kuwa na uhakika wa kipato amekusidia kuanzisha mfuko maalum wa vijana (Saccos) waendesha pikipiki  na akina mama wajasiliamali ambapo atachangia mfuko uwe na uwezo w...

MHE. NDEJEMBI AWAHAKIKISHIA WAKAZI WA KIGAMBONI UMEME WA UHAKIKA*

Image
📌Afanya Ziara katika Kituo cha Dege  📌Aelekeza hatua za haraka kuchukuliwa kunusuru hali ya umeme Kigamboni 📌Umeme wa Megawati 22 kupatikana kwa hatua za haraka  📌Upanuzi wa Kituo cha Dege wafikia asilimia 60  Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ndani ya Mkoa wa kitanesco wa Kigamboni na kuagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kuhakikisha hali ya umeme katika Mkoa wa Kigamboni inaboreshwa na kuwapa wakazi wa eneo hilo huduma ya uhakika alipotembelea Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza umeme cha Dege tarehe 29 Novemba, 2025. “Leo tumekuja kuona ni namna gani Shirika letu la TANESCO linaweza kutatua changamoto hii kwa haraka zaidi na wameweka mipango mizuri ya muda mrefu katika kuhakikisha wanawezesha kupatikana kwa umeme wa uhakika kwa kujenga na kukiongezea nguvu Kituo cha Dege kwa kuweka transfoma ya MVA 120”, ameeleza Mhe. Ndejembi.  Ili kukabiliana na changamoto ya huduma ya umeme iliyopo kwa haraka, Shirika limekuja na suluhi...

WAZIRI MAVUNDE AWAASA WAMILIKI WA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA UCHIMBAJI*

Image
●  Maboresho ya Kanuni za Haki Madini za Mwaka 2025 yaongeza ufanisi kwa wenye maduara na kupunguza migogoro, ●  Wamiliki wa Leseni za Utafiti wasioendeleza Leseni kufutiwa Leseni ●  Vikundi vya vijana na wanawake  vyaendelea kunufaika na utekelezaji wa Programu ya MBT, ●  Waziri Mavunde asisitiza amani na utii wa Sheria kwa wachimbaji wadogo, 📍Nyang'wale, Geita Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akiwa ziarani Wilayani Nyang'wale amewaasa na kuwataka wamiliki wa leseni za uchimbaji wa madini kuzingatia Sheria ya Madini Sura ya 123 na Kanuni zake katika utekelezaji wa majukumu yao. Akizungumza katika ziara hiyo iliyofanyika kwenye eneo la mgodi wa Kasubuya wilayani Nyang’hwale, Waziri Mavunde amesema wachimbaji wadogo kwa sasa wanachangia zaidi ya asilimia 40 ya mapato yatokanayo na sekta ya madini, akibainisha kuwa mchango wao unaendelea kuongezeka kutokana na maboresho makubwa ya Sheria, Kisera na Kiutendaji yanayofanywa na Serikali. Waziri Mavunde a...

MELI KUBWA YA MZIGO KUTOKA IRAN YATIA NANGA BANDARI YA TANGA.

Image
Na,Agnes Mambo,Tanga.. Mkuu wa mkoa wa Tanga amesema wataendelea kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara na nchi ya Irani Kwa kufanyabiasha ikiwemo kubadilishana bidhaa Kwa bei nafuu Kwa kuanzisha VIWANDA vidogo vidogo vya machine za uzalishaji bidhaa mbalimbali. Aidha Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian ameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya sita Kwa maboresho ya Bandari ya Tanga yameendelea kuzaa matunda kutokana na kupokea Meli kubwa za mizigo mara kwa mara na mapato ya kiuchumi kuongezeka mara dufu. Pongezi hizo amezitoa Novemba 28 akiwa katika Bandari ya Tanga baada kupokea Meli kubwa ya mizigo yenye tani elfu 13 kutoka nchini Irani iliyobeba makontena 463 kati ya hayo makontena 261 mizigo ya ndani na makontena 182 ambayo yanasafirishwa kwenda nchi za Afika Mashariki. Kwa upande wake kaimu Meneja wa Bandari,Peter Milanzi amesema Kwa mara ya kwanza Bandari ya Tanga kuandika historia ya kupokea Meli kubwa ya Moja Kwa Moja kutoka nchini Irani iliyofahamika Kwa Jina la ...

*MAWAKALA WA UTALII KUTOKA UINGEREZA WATEMBELEA TANZANIA KUONA VIVUTIO VYA UTALII.

Image
Mwezi mmoja baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu nchini Tanzania wadau wa utalii duniani wanaendelea kumiminika ambapo mawakala  wakubwa wa utalii kutoka Nchini Uingereza wako nchini kutembelea hifadhi mbalimbali ili kuona vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji kwa lengo la kuiuza nchi katika soko la Ulaya. Kiongozi wa Mawakala hao Debbie Mayger ambae na ujumbe wake wamewasili eneo la hifadhi ya Ngorongoro leo tarehe 29 Novemba, 2025 ameeleza kuwa  wamekuja Tanzania kutembelea hifadhi kuona utajiri wa vivutio vya utalii, urithi wa utamaduni, spishi za wanyamapori, manthari na uhifadhi asilia, fukwe kwenye hifadhi za bahari, pamoja na mila na tamaduni za Kitanzania. “Tumekuwa tukisikia habari nyingi kuhusu Tanzania, tuna soko kubwa la watalii katika nchi za ulaya na wanapenda utalii wa kuona wanyamapori mbalimbali, Kreta ya Ngorongoro, urithi wa dunia uliopo Ngorongoro, Jiopaki ya Ngorongoro Lengai, tamaduni ndani ya hifadhi, utunzaji na uhifadhi wa mazingira, ukarimu pamoja...

TANZANIA SHINES IN TOURISM: MINISTER KIJAJI MEETS INTERNATIONAL TOURISTS AT NGORONGORO”

Image
The Minister for Natural Resources and Tourism, Hon. Dr. Ashatu Kijaji (eighth from left), is pictured with international tourists she met at the Ngorongoro Conservation Area entrance (Loduare Gate) during an inspection tour of tourism activities in the area. Dr. Kijaji was accompanied by the Deputy Minister for Natural Resources and Tourism, Hon. Hamad Chande (sixth from left), the Permanent Secretary of the Ministry, Dr. Hassan Abbasi (left), and the Conservation Commissioner for the Ngorongoro Conservation Area, Mr. Abdul-Razaq Badru (right). During the visit, Minister Kijaji assured the tourists that Tanzania remains a peaceful and welcoming destination and continues to implement the directives of the President as well as the CCM government manifesto in serving Tanzanians. Several ministers have already begun implementing the manifesto following the conclusion of the general elections on October 29, 2025.

MRADI WA UMEME KISHAPU KIELELEZO CHA ONGEZEKO LA UZALISHAJI UMEME NCHINI – DC KISHAPU

Image
📌Mradi wa umeme wa jua wafikia asilimia 84 ya utekelezaji 📌MD Twange aagiza ukamilishwe ifikapo Januari 15, 2026 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amesema mradi wa umeme unaozalishwa kwa nguvu ya jua ni kielelezo cha ongezeko la uzalishaji wa umeme nchini  ikiwa ni dhamira ya Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuongeza uzalishaji umeme hadi kufikia jumla ya megawati 8000 ifikapo mwaka 2030. Mhe. Masindi aliyasema hayo Novemba 28, 2025, alipoambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, kukagua maendeleo ya Mradi wa kuzalisha umeme wa jua unaotekelezwa wilayani humo. Amesema mradi huo sio tu utakuwa na faida kwa wananchi wa Mkoa wa Sinyanga pekee bali hadi katika mikoa ya Jirani ambapo pia amesema zaidi ya wananchi 1,200 waliokuwa wakiendesha shughuli zao katika eneo la Mradi tayari  wamelipwa fidia na kwamba jamii imeupokea mradi kwa mtazamo chanya na imekuwa mstari wa mbele kulinda miundombinu. “Mradi huu ni teg...

DKT. KIJAJI ASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UHIFADHI*

Image
Na Kassim Nyaki, Karatu. Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameelekeza taasisi za uhifadhi kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori ili kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori. Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo leo tarehe 28 Novemba, 2025 wakati akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wakati wa ziara ya kujitambulisha kwenye taasisi na kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo. Katika kikao hicho Mhe. Waziri Kijaji  ameelekeza kuwa kila taasisi ni lazima iwekeze kwenye teknolojia za kısasa ili kuimarisha ulinzi wa rasilimali za nchi ambazo ni kichocheo cha wageni mbalimbali kutembelea nchi yetu. Kwa upande wake naibu waziri wa wizara hiyo Mhe.Hamad Hassan Chande amewataka watumishi katika sekta ya uhifadhi na utalii kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubunifu katika kuwahudumia wageni. Akiwatambulisha viongozi hao kwa menejimenti ya Ngorongoro Katib...

REA IMEFANYA KAZI KUBWA YA KUFIKISHA HUDUMA ZA NISHATI VIJIJINI - WAZIRI NDEJEMBI

Image
*📌Asisitiza ubunifu katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia* *📌Mradi wa vitongozi 9,000 mbioni kuanza* 📍Dodoma Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kufikisha umeme kwenye vijiji na maeneo ya pembezoni mwa miji iliyopelekea kukuza shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo. Pongezi hizo zimetolewa leo Novemba 28, 2025 wakati Mhe. Ndejembi alipokutana na kuzungumza na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) pamoja na Menejimenti ya REA kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na vitongojini pamoja na utekelezaji wa Mkakati wa nishati safi ya kupikia katika kikao kilichofanyika Ofisi za Makao Makuu ya REA jijini Dodoma.  "REA imefanya kazi kubwa na nzuri sana hapa nchini hususan katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Kipekee nachukua fursa hii kuipongeza sana Bodi ya REA, Menejimenti  na Wafanyakazi kwa ujumla kwa kufanya kazi kubwa ya kupeleka umeme katika vijijini vyote nchini, " Amesema Mhe. Ndeje...

WATENDAJI MSIKWAMISHE SHUGHULI ZA VIJANA - NANAUKA

Image
Na. OR- MV, Songea Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka  ameendelea na ziara yake maalum ya kukutana na kuzungumza na Vijana katika Mkoa wa Ruvuma ambapo ameonya dhidi ya watendaji wa Serikali  wanaokwamisha shughuli za Vijana kuwa hawatavumiliwa. Akiwa Wilayani Songea leo Ijumaa (28 Novemba 2025) amekutana na Vijana wajasiliamali wanaofanya shughuli katika Soko la Bombambili na Stendi ya magari ya Ruhuwiko ambapo amesikiliza mawazo na ushauri wa Vijana ikiwemo kutatua kero . Katika mazungumzo hayo  Vijana wa Manispaa ya Songea wamelalamikia ucheleweshaji wa upatikanaji mikopo toka Halmashauri, mazingira yasiyoridhisha ya kufanyia biashara ikiwemo kero ya tozo na ushuru. Waziri Nanauka amewaeleza  Vijana hao kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anayo dhamira ya dhati kuona Vijana wanashiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa nchi hivyo kuwasihi waitunze amani na kutumia njia ya mazungumzo kutatua changamoto ndio maana akaamua  kuundwa kwa Wizara...

MIKOPO IWE CHACHU YA KUKUA KIUCHUMI NA KUZITUNZA FAMILIA ZENU – MHE. MARYPRISCA

Image
Na Jackline Minja MJJWM, Dodoma. Serikali imeendelea kuanzisha  Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi  kuanzia ngazi ya Vijiji/Mtaa, Kata, Wilaya na Mkoa ambapo  Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025, jumla ya Majukwaa 15,147 yameanzishwa, ambayo yameleta chachu kwa wanawake ya kujifunza masuala ya ujasiriamali, elimu ya fedha na uwekezaji. Hayo yamesemwa na Naibu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi MaryPrisca Mahundi wakati akizungumza na wanavikundi vya malezi na matunzo ya watoto Kata ya Ihumwa Jijini Dodoma. Mahundi amesema katika eneo la fursa za kiuchumi, Wizara inaratibu na kusimamia jukumu la kuwezesha kiuchumi wafanyabiashara ndogondogo na wao wakiwa miongoni mwao watatambuliwa na kuwasajili na kutoa mikopo yenye masharti nafuu, katika zoezi linalosimamiwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa TEHAMA pamoja na Maafisa Biashara ngazi ya Mikoa na Halmashauri. “Tangu zoezi hili lilipoanza mwezi Februari, 2024 hadi kufikia ...