TIMU YA WANAWAKE NGORONGORO YAKAA MGUU SAWA MASHINDANO YA SHUMMUTA MOROGORO.*



Timu ya mpira wa Netiboli na mpira wa wavu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewasili mkoani Morogoro tarehe 25 Novemba 2025, imeendelea na program ya mazoezi katika viwanja vya Bwalo la JKT ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya SHIMMUTA ambayo  yameanza tarehe 25 Novemba, 2025.

Akizungumza wakati wa mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo yanayohusisha timu za mashirika mbalimbali, kocha wa timu ya Ngorongoro, Mathias Evarist ameeleza kuwa wachezaji wako tayari kuonyesha uwezo wao na kupambana katika michezo iliyoanza tarehe 25 Novemba hadi 06 Desemba 2025.

Kwa mujibu wa Afisa Michezo Mwandamizi wa NCAA Bw. Yotham Gitige, katika mashindano hayo Ngorongoro inashiriki michezo ya mpira wa Netiboli, Mpira wa wavu na mchezo wa Riadha





Comments

Popular posts from this blog

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

DC Mnzava akabidhiwa hati ya Pongezi na CCM kwa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani

OFISI ZA MADINI NCHINI ZATAKIWA KUIMARISHA ELIMU YA ULIPAJI KODI*