MAKAMU WA RAIS DKT EMMANUEL NCHIMBI AKABIDHIWA OFISI NA DKT PHILIP MPANGO



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amempongeza na kumshukuru Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa mchango aliyoutoa wakati wa kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Sita.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa makabidhiano ya Ofisi ya Makamu wa Rais, yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. Amesema kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha kwanza cha Awamu ya Sita, ambayo ilitoa urahisi wakati wa ufanyaji kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Makamu wa Rais amesema ataendeleza jukumu la kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwezo wake wote ili kutekeleza vema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuwaletea wananchi maendeleo.
 

Pia amemsihi, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Philip Mpango kuendelea kutoa mchango wake pale utakapohitajika, katika utekelezaji wa sera mbalimbali za Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwemo masuala ya uchumi wa buluu.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Philip Mpango amempongeza Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa nafasi hiyo muhimu na kumsihi kutekeleza vema majukumu ya kuwa mshauri namba moja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia amemsihi kutumia hekima na unyenyekevu wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

Novemba 04, 2025

Ikulu – Chamwino.




Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO