DKT. KIJAJI ASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UHIFADHI*



Na Kassim Nyaki, Karatu.

Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameelekeza taasisi za uhifadhi kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori ili kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.

Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo leo tarehe 28 Novemba, 2025 wakati akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wakati wa ziara ya kujitambulisha kwenye taasisi na kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.

Katika kikao hicho Mhe. Waziri Kijaji  ameelekeza kuwa kila taasisi ni lazima iwekeze kwenye teknolojia za kısasa ili kuimarisha ulinzi wa rasilimali za nchi ambazo ni kichocheo cha wageni mbalimbali kutembelea nchi yetu.


Kwa upande wake naibu waziri wa wizara hiyo Mhe.Hamad Hassan Chande amewataka watumishi katika sekta ya uhifadhi na utalii kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubunifu katika kuwahudumia wageni.

Akiwatambulisha viongozi hao kwa menejimenti ya Ngorongoro Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuharakisha mipango ya serikali inatekelezwa.

Mapema viongozi hao wa wizara walipata fursa ya kukagua ujenzi wa Makao makuu ya mamlaka hiyo, kukagua shughuli za utalii katika lango La Loduare na Makumbusho ya kihistoria ya Urithi ya Jiopaki ya Ngorongoro (Urithi Geo Museum)



Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO