MABAKI YA MWILI WA MTANZANIA JOSHUA MOLLEL YAWASILI NCHINI TANZANIA



Mabaki ya mwili wa Kijana Joshua Mollel aliyeuwawa nchini Israel na wapiganaji wa HAMAS Oktoba 07, 2023 yamewasili leo Novemba 19, 2025 katika kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).

Mabaki ya mwili huo yamepokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania ukiongozwa na  Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa na Balozi Silima Haji Kombo. 

Mabaki ya Kijana Joshua Mollel yanatarajiwa kuzikwa   kesho  Novemba 20,  2025 mtaa wa Njiro, katika kata Orkesumet Wilaya ya Simanjiro,  Mkoani Manyara.




Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO