MAKAMU WA RAIS DKT EMMANUEL NCHIMBI AWASILI ZAMBIA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Jijini Lusaka nchini Zambia leo Novemba 19, 2025.

Makamu wa Rais anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Ukarabati Mkubwa wa Reli ya TAZARA itakayofanyika tarehe 20 Novemba 2025 Jijini Lusaka.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Makamu wa Rais amepokelewa na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Dkt. Elijah Muchima, Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, Maafisa waandamizi wa Jamhuri ya Zambia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoandaliwa kwa heshima yake.

Pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja pamoja Mkurugenzi Mkuu TASAC Bw. Mohamed Salum.

Imetolewa na 

Ofisi ya Makamu wa Rais

19 Novemba 2025

Lusaka - Zambia.





Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO