MENEJA WA LUSHOTO EXECUTIVE LODGE AELEZA UZURI WA UTALII WA USANBARA LUSHOTO.
Meneja wa Lushoto Executive Lodge, Bw. Sifa Mwambire, amewakaribisha wageni wa ndani na nje ya nchi kutembelea wilaya ya Lushoto na kufurahia huduma bora pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika eneo hilo lenye mandhari ya kipekee. Akizungumza hivi karibuni, Bw. Mwambire alisema kuwa Lushoto Executive Lodge imejipambanua kwa kutoa huduma za kiwango cha juu katika mazingira tulivu na salama, huku ikilenga kuwahakikishia wageni faraja, ukarimu na mapumziko yenye ubora. Alisema lodge hiyo ni mahali sahihi kwa wageni wanaotafuta utulivu na huduma bora za malazi. Bw. Mwambire, ambaye pia ni mmoja wa wadau na wadhamini wakubwa wa walkathon iliyofanyika Magamba wilayani Lushoto, alisema ushiriki wao katika kudhamini tukio hilo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kukuza utalii na kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika wilaya hiyo. Alibainisha kuwa Lushoto imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ikiwemo milima ya Usambara, misitu ya asili, maporomoko...