MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO NCAA INASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA KASKAZINI ARUSHA
Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) inashiriki Maonesho ya Wakulima NaneNane Kanda ya Kaskazini katika viwanja vya Themi Njiro Arusha, Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma na Uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya kwa ajili ya kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu vivutio vya utalii, urithi wa Utamaduni na Mambo Kale, Uhifadhi shirikishi, maendeleo ya jamii pamoja na fursa za uwekezaji zinazopatikana katika hifadhi ya Ngorongoro.
Tembelea banda letu la NCAA uweze kujua mengi kuhusu hifadhi ya Ngorongoro ambayo ni kivutio namba moja cha utalii barani Afrika na moja ya chaguo bora la wageni wa Safari waliotembelea kwa mujibu wa mtandao wa TripAdvisor
Maonesho ya NaneNane yalianza rasmi Agosti 01, 2025 na kaulimbiu ya mwaka huu ni “Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo,mifugo na uvuvi 2025” na yanatarajiwa kutamatika mnamo Agosti 08, 2025.
Comments
Post a Comment