WANANCHI WAENDELEA KUMIMINIKA ENEO LA HAFLA YA UZINDUZI WA BWAWA LA MWALIMU NYERERE (JNHPP)
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini wameendelea kumiminika katika eneo la hafla ya uzinduzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), wakishuhudia tukio hilo muhimu katika historia ya maendeleo ya sekta ya nishati nchini.
Hafla hiyo inafanyika leo, huku wananchi na wageni mbalimbali wakifika katika eneo la tukio kushiriki katika tukio hilo kubwa linalohusisha uzinduzi rasmi wa mradi huo wa kimkakati wa kuzalisha umeme.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye anatarajiwa kuzindua rasmi Bwawa la Mwalimu Nyerere na kuzungumza na wananchi pamoja na wadau mbalimbali watakaoshiriki katika hafla hiyo.




Comments
Post a Comment