DC RUKIA ATEMBELEA MABANDA YA MAONESHO YA 88 YA NANENANE ARUSHA
DC RUKIA ATEMBELEA MABANDA YA MAONESHO YA 88 YA NANENANE ARUSHA
Na Musa Mathias,
Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Rukia Zuberi, ametembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya 88 ya Nanenane Kanda ya Kaskazini, yanayoendelea jijini Arusha, akijionea teknolojia, ubunifu na huduma zinazotolewa na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.
Katika ziara hiyo, Mhe. Rukia alipata maelezo kuhusu maendeleo katika sekta za kilimo, ufugaji na elimu ya juu, huku akielezwa namna teknolojia za kisasa zinavyochangia kuongeza uzalishaji, tija na thamani ya mazao na bidhaa zinazozalishwa nchini.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda hayo, aliwataka wananchi na washiriki wa maonesho kutumia fursa ya Maonesho ya Nanenane kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuhamasisha matumizi ya teknolojia zinazochochea maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuendeleza uzalishaji kupitia viwanda vya ndani na kuongeza thamani ya bidhaa za Tanzania, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuzalisha ajira, kukuza uchumi na kuimarisha ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mhe. Rukia amesema Maonesho ya 88 ya Nanenane yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha wadau wa maendeleo, kuonesha mafanikio ya sekta za uzalishaji na kuhamasisha matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika safari ya kujenga uchumi imara wa Tanzania.
#KipeoOnlineMedia #Habari #Tanzania #News #Update
Asante kwa kusoma Kipeo Online Media. Tembelea kipeoonlinemedia.blogspot.com kwa habari zaidi, Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa youtube.com/@kipeoonlinemedia?si=vZ45foO1hBmK1xvX
karibu sana.




Comments
Post a Comment