CHEREKO CHEREKO BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO.*



Kamati tendaji ya Baraza la Wafugaji  tarafa ya Ngorongoro imekutana leo tarehe 18 Agosti, 2026 ambapo pamoja na mambo mengine imechambua na kupitisha orodha ya majina ya wanafunzi wa kidato cha tano kutoka kata 11 za tarafa ya Ngorongoro wanaofadhiliwa na Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro

Majina ya wanafunzi wanaofadhiliwa na Ngorongoro yanatokana na mapendekezo ya  kata zote 11 zenye Vijiji 25 ambapo kila kata inachagua wanafunzi watatu (03) ambapo wanapata fursa hiyo ikiwa ni hatua ya kuendelea kuboresha uhusiano kati ya Ngorongoro na Jamii inayoishi ndani ya hifadhi

Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa sambamba na kusaidia huduma  za elimu kwa wanafunzi wa tarafa ya Ngorongoro, katika kipindi cha wiki moja ijayo itafanyika tathmini ya mahitaji ya maji na barabara zenye changamoto ambapo Ngorongoro inatarajia kuchimba visima  saba  (07) na kukarabati mtandao wa barabara katika maeneo ya hifadhi ili kuhudumia wananchi na watalii.

Aidha Ngorongoro kwa kushirikiana na makampuni ya simu inatarajia kuimarisha huduma ya Mawasiliano ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2026 maeneo mengi ndani ya hifadhi huduma  ya mawasiliano itakuwa imeimarika.

Kamati tendaji ya Baraza la wafugaji wa Tarafa ya Ngorongoro inaundwa na waheshimiwa madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, Viongozi wa mila na wawakilishi wa wanawake, Mhifadhi NCAA,wawakilishi wa vijana.

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO