WAZIRI WA NISHATI MHE DEOGRATIUS NDEJEMBI AKIKAGUA MABANDA YA WADAU WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb.), akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, pamoja na viongozi wengine, wakikagua mabanda ya wadau wa nishati safi ya kupikia waliohudhuria Mdahalo wa Nishati Safi unaofanyika katika Hoteli ya Kwanza-Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja-Zanzibar, leo tarehe 11 Agosti 2026.
Mdahalo wa Nishati Safi umeandaliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) kuelekea Tamasha kubwa la Kizimkazi Festival.
Viongozi hao wameambatana na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Reuben Kwagilwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Mhandisi Felchesmi Mramba, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kati, Mhe. Rajab Ali.


Comments
Post a Comment