DC RUKIA AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO, ASISITIZA KULINDA AMANI.

DC RUKIA AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO, ASISITIZA KULINDA AMANI.


Mwanga, Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Rukia Zuberi, amesisitiza kuwa amani na usalama ni nguzo kuu ya maendeleo ya Taifa, akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudumisha utulivu na kulinda maendeleo ya Wilaya hiyo.

Ameyasema hayo Agosti 5, 2026, wakati akifungua mafunzo ya awali kwa askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo) Kundi la 32/26 yaliyofanyika katika Kijiji cha Kituri, Kata ya Kileo, Tarafa na wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro. 

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi, Mhe. Rukia alisema kuwa pasipo amani na usalama, jamii haiwezi kupata ustawi wala kufaidika kikamilifu na huduma muhimu za kijamii ikiwemo elimu, afya na miundombinu ya maendeleo.
"Amani na usalama ni msingi wa maendeleo ya Taifa. Pasipo utulivu na usalama, jamii haiwezi kupata ustawi; huduma muhimu kama elimu, afya na nyingine za kijamii haziwezi kutolewa kwa ufanisi," alisema Mhe. Rukia.

Aidha, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kujifunza kwa bidii, kuzingatia nidhamu na kujijengea uwezo utakaowawezesha kulitumikia Taifa kwa weledi, uzalendo na uadilifu katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao.

Mhe. Rukia amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuimarisha ulinzi shirikishi, hatua ambayo itachangia kuifanya Wilaya ya Mwanga kuendelea kuwa eneo lenye amani, utulivu na mazingira rafiki kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mwisho.

#KipeoOnlineMedia #Habari #Tanzania #News #Update Asante kwa kusoma Kipeo Online Media. Tembelea kipeoonlinemedia.blogspot.com kwa habari zaidi, Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa youtube.com/@kipeoonlinemedia?si=vZ45foO1hBmK1xvX karibu sana.

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO