SAME WAZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA CHANJO YA POLIO, WATOTO 85,677 KUFIKIWA.

SAME WAZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA CHANJO YA POLIO, WATOTO 85,677 KUFIKIWA.



Na Musa Mathias, 
Same, Kilimanjaro. 

Serikali wilayani Same imewasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka 10 kupata chanjo ya Polio ya matone, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo hatari huku Wananchi wakisisizwa kutosikiliza taarifa zinazopotosha kuhusu usalama wa chanjo, bali kuzingatia elimu na maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya.

Hayo yameelezwa Agosti 27, 2026 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Same, Bi. Mamndolwa Gembe, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa awamu ya kwanza ya Chanjo ya Polio ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka 10 wilayani humo mkoani Kilimanjaro, ambapo amesema Serikali ina dhamira ya dhati kuhakikisha watoto wanakuwa salama na wenye afya njema kupitia huduma mbalimbali za afya, ikiwemo chanjo ya Polio. 
Bi. Mamndolwa amesema ugonjwa wa Polio ni hatari kwa kuwa hushambulia mfumo wa fahamu na unaweza kusababisha kupooza kwa mwili, ulemavu wa kudumu na hata kifo, Amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wenye umri chini ya miaka 10 wanapata chanjo hiyo, akisisitiza kuwa chanjo ya Polio ni salama na ina umuhimu mkubwa katika kumkinga mtoto dhidi ya ugonjwa huo.

“Ugonjwa wa Polio ni hatari sana kwani unashambulia mfumo wa fahamu na unaweza kusababisha kupooza kwa mwili na hata kifo. Tuhakikishe watoto wetu wenye umri chini ya miaka 10 wanapata chanjo hii ya Polio, kwa sababu chanjo hii ni salama,” amesema Bi. Mamndolwa.
Aidha, amewataka wahudumu wa afya, watendaji wa Serikali, wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na walimu kuongeza juhudi za kutoa elimu na hamasa kwa wananchi katika maeneo yote, Amesema ushirikiano wa wadau hao ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata uelewa sahihi kuhusu umuhimu wa chanjo na hivyo kuwawezesha wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo kwa ajili ya kuwalinda dhidi ya Polio.

Kampeni ya Chanjo ya Polio Awamu ya Kwanza inafanyika katika mikoa minane nchini Tanzania kuanzia Agosti 27 hadi 30,2026, ikiwa na lengo la kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa wa Polio kutokana na milipuko iliyotokea katika nchi jirani. Kampeni hiyo inawalenga watoto wote wenye umri chini ya miaka 10, huku Wilaya ya Same ikitarajia kuwafikia jumla ya watoto 85,677 kwa ajili ya kupata chanjo hiyo.









#KipeoOnlineMedia #Habari #Tanzania #News #Update Asante kwa kusoma Kipeo Online Media. Tembelea kipeoonlinemedia.blogspot.com kwa habari zaidi, Subscribe Channel yetu ya Youtube hapa youtube.com/@kipeoonlinemedia?si=vZ45foO1hBmK1xvX karibu sana.

Comments

Popular posts from this blog

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

DC Mnzava akabidhiwa hati ya Pongezi na CCM kwa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani

OFISI ZA MADINI NCHINI ZATAKIWA KUIMARISHA ELIMU YA ULIPAJI KODI*