TANAPA YANADI VIVUTIO VYAKE NA FURSA ZA UWEKEZAJI - SABASABA 2025.*
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linashiriki Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii, fursa za uwekezaji na kuelimisha umma umuhimu wa kuhifadhi Maliasili kwa faida ya Tanzania na dunia kwa ujumla. Katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi uhifadhi wa mimea ni jambo ambalo TANAPA pia italipa kipaumbele ili kuwa na mazingira rafiki na salama kwa binadamu na wanyamapori.
Karibu we mwananchi katika Banda la TANAPA upate elimu ya Uhifadhi, ujue umuhimu wa utalii na ofa mbalimbali za kutembelea Hifadhi za Taifa katika kipindi hiki cha Msimu wa Sabasaba.
Aidha, shirika hilo litaendelea kutumia jukwaa hilo kuonesha jitihada mbalimbali zilizofikiwa katika kudumisha mahusiano mema na jamii zinazozunguka hifadhi hizo zilizohifadhi tunu mujarabu za Taifa.
Maonesho hayo yaliyoanza rasmi June 28, 2025 yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Julai 04, 2025 huku kauli mbiu ikiwa ni *“SabaSaba Fahari ya Tanzania”*
Comments
Post a Comment