WAZIRI MKUU ATEMBELEA KITUO CHA MALEZI YA WATOTO, SANGANIGWA, KIGOMA*


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 13, 2025 ametembelea kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Sanganigwa kilichopo mjini Kigoma, kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Kigoma.

Akizungumza na watoto na walezi wa kituo hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuwalea kimwili na kiroho watoto wenye mahitaji maalum nchini.

“Kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ninalishukuru kanisa katoliki jimbo la Kigoma, mtu mmoja mmoja na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa Serikali katika kuwalea watoto wetu, hakika mnafanya jambo kubwa na lakumpenda Mungu na wanadamu”


Akisoma taarifa ya kituo hicho kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Kituo hicho Keneth Hageze amesema kuwa kilianzishwa mwaka 1995 na mpaka sasa kimehudumia watoto 1309.

Mheshimiwa Majaliwa alitoa Mchele, Maharage, Mafuta, Sukari pamoja na Taulo za kike.


 

Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO