NYUMBA ZA WALIMU KICHOCHEO KUINUA TAALUMA, USIMAMIZI WA SHULE
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
IMEELEZWA kuwa ujenzi wa nyumba za walimu katika na shule wanazofundishia ina faida kubwa katika kupunguza usumbufu kwa walimu kuishi mbalimbali na shule hivyo kusaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi na kuinua taaluma.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa, Ismail Alli Ussi alisema hayo wakati mwenge wa uhuru ukizindua nyumba moja ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia mbili katika shule ya Sekondari Msambara Halmashauri ya mji wa Kasulu wilayani Kasulu
Ussi alisema kuwa walimu kuishi karibu na shule kunasaidia kuwa na mahudhurio mazuri shuleni, muda mzuri wa kujiandaa kwa ajili ya kufundisha lakini inaondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu na wakati mwingine kushindwa kufika shuleni wakati wakati wa mvua hivyo uwepo wa nyumba hizo ni muhimu katika kusimamia taaluma.
Kutokana na umuhimu huo alisema kuwa serikali itaendelea kujenga nyumba Zaidi nchi nzima kuhakikisha walimu wanaishi katika nymba nzuri na bora na karibu na shule ili kufurahia kazi yao ya kufundisha badala ya kuuona ualimu kama adhabu.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa wilaya Kasulu, Isack Mwakisu alisema kuwa halmashauri kupitia mapato ya ndani, kupitia Amiradi mbalimbali ya elimu ukiwemo Mpango wa maendeleo ya shule za sekondari, Mradi wa kuimarisha elimu ya sekondari (SEQUIP) na wahisani mbalimbali imekuwa ikiboresha miundo mbinu ya shule ili kurahisisha katika kufundisha na usimamizi wa shule.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo Mkuu wa shule ya sekondari Msambara, Mwalim Elima Mgina alisema kuwa kiasi cha shilingi Milioni 110 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huo kupitia Mradi wa kuimarisha shule za sekondari (SEQUIP).
Comments
Post a Comment