MZEE MAKAMBA AMUOMBEA KURA RAIS SAMIA. MGOMBEA UBUNGE WA CCM BUMBULI


Na Ashrack Miraji kipeo online 

Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Mzee Yusuf Makamba amewaomba wananchi wa Jimbo la  Bumbuli mkoani Tanga kumchagua mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Mhandisi Ramadhani Singano na madiwani wote wa chama hicho.

Makamba amesema hayo leo Septemba 15, 2025 kwa njia ya simu kwenye mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi uliofanyika Lushoto eneo la Soni.

Mzee makamba amesema anaimani na wagombea wote wa CCM na alipenda kuhudhuria mkutano huo ila tatizo ni changamoto ya afya yake.

Dk Nchimbi alimpigia simu Mzee Makamba akiwa jukwaani ndipo alipozungumza na kuwaombea kura wagombe wote huku akiwaomba wananchi wa mkoa wa Tanga wasimuangushe katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 29, 2025.






 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO