WATEJA WAKUBWA WA HOTELI MOROGORO WAKAMATWA KWA WIZI WA UMEME*



πŸ“*Ni katika operesheni maalum ya ukaguzi inayofanywa na TANESCO Nchi nzima*

πŸ“*TANESCO yasisitiza zoezi ni endelevu na kutangaza kiama kwa waolihujumu Shirika*

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewakamata wateja wakubwa wawili mkoani Morogoro ambao ni PH Hotel na Igombe Hotel wakijihusisha na wizi wa umeme ambapo waligundulika kuchepusha nyaya kwenye mita zao aina ya T2 na hivyo kutumia umeme bila kulipa gharama yoyote jambo linalolikosesha Shirika mapato.

Wateja hao wamekamatwa wiki hii ikiwa ni kati ya wateja 14 waliokamatwa katika operesheni hiyo inayohusisha wataalamu wa mita kutoka Makao Makuu TANESCO wakishirikiana na ofisi ya Mkoa wa TANESCO Morogoro Kaskazini.

Timu hiyo ya ukaguzi ilifika katika maeneo ya Msamvu, Morogoro, ambako hoteli hizo zipo, na kufanikisha kubaini hujuma hizo kwa ushirikiano wa viongozi wa Serikali za Mtaa wa White House pamoja na Jeshi la Polisi.

Aidha, Shirika linaendelea kuimarisha ukaguzi na kushirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wote wanaobainika kujihusisha na vitendo hivyo vinavyolikosesha Shirika mapato.



Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO