MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAONGEZEKA NCHINI*



📌 *Mhandisi Mramba asema yamefikia asilimia 20.3  kutoka asilimia 6.9 ya mwaka 2021*

📌 *Lengo ni kufikia asilimia 80 ifikapo 2034*

📌 *Apongeza juhudi za Rais Samia katika kuwezesha upatikanaji wa nishati safi, salama na nafuu kwa Watanzania*

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha.Felchesmi Mramba ameeleza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia nchinj yameongezeka kutoka asilimia  6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 20.3 huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 80 ndani ya miaka 10, ambapo hadi sasa imebakia miaka 9.

Mha. Mramba ameyasema hayo Septemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kongamano la  Nishati Safi ya Kupikia lililoandaliwa na kampuni ya Mwananchi kwa ushirikiano  na Wizara ya Nishati pamoja na wadau mbalimbali likibebwa na kaulimbiu ya  ‘Nishati safi ya Kupikia Okoa Maisha, Linda Mazingira.

Akizungumza  wakati wa uzinduzi huo, Mha. Mramba amesema  “Nishati Safi ya Kupikia siyo jambo la kinadharia bali ni jambo linalohusu maisha, mazingira na uchumi huku msingi wake mkuu ukiwa ni kulinda afya, mazingira pamoja na maendeleo jumuishi.” 

Aidha, Mhandisi Mramba ameendelea kuwahamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia akikumbusha kuwa, takwimu zinaonesha kuwa takribani watanzania 33,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na uvutaji wa moshi unaotokana na matumizi ya nishati isiyo safi ikiwemo kuni na mkaa.

Ameeleza kuwa kutokana na athari hizo   Serikali chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia 2024–2034 uliozinduliwa mwezi Mei 2024 ambao utawezesha asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia.

Sanjari na hayo, Mha. Mramba amemshukuru Rais,  Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi ya kupikia kitaifa na kimataifa kwa Uongozi wake wa mfano na dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha kila Mtanzania anatumia nishati safi, salama na nafuu ya kupikia.





Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO