TANESCO YAUNGANA NA WAOMBOLEZAJI KATIKA IBADA YA FARAJA KUFUATIA VIFO VYA WATUMISHI WAKE



Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) jana tarehe 16/9/2025 waliungana na familia, ndugu jamaa na marafiki katika ibada ya faraja ya kuwaaga  watumishi wenzao, marehemu Fransic Kaggi na Elineema Kaggi, pamoja na ndugu zao Janemary Kaggi, Mary Kaggi na Joshua Kaggi waliopoteza maisha katika ajali mbaya ya gari iliyotokea tarehe 14 Septemba 2025, katika eneo la Msata mkoani Bagamoyo.

Ibada hiyo iliyofanyika katika kanisa la kkkt kijitonyama jijini Dar es salaam ilikua  ya kuaga miili ya marehemu hao wa familia moja ambapo mazishi yanafanyika leo tarehe 17 Septemba 2025.

Akitoa salaamu za rambirambi  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji Umeme wa TANESCO kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO ameeleza  kusikitishwa kwake na msiba huu mzito, na kusema kuwa Shirika limepoteza nguvu kazi muhimu katika ujenzi wa Taifa.

'' kwakweli msiba huu ni mkubwa sana na tumeupokea kwa mshtuko mkubwa kutokana na kwamba watumishi hawa walikua nguvu kazi muhimu na walifanya kazi kwa uhodari mkubwa na hivyo pengo hilo ni gumu kuzibika na hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Twange natoa pole sana kwa familia ndugu na jamaa na tuko pamoja katika wakati huu mgumu''

Maziko ya watumishi hawa yanafanyika leo katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.





Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO