SAMIA SULUHU AOMBEWA KURA KWA WANANCHI WA JIMBO LA TANGA KEENYE UZINDUZI WA KAMPENI.
Na,Agnes Mambo,Tanga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdulrahaman amesema amekuja katika mkutano wa hadhara wa wananchi kumuombea kura Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na mgombea, Ubunge,madiwani kwenye uzinduzi wa kampeni Jimbo la Tanga mjini
Ameomba ridhaa Kwa Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi ambapo alikuwa mgeni rasmi Septemba 62025 .
Amewataka Wananchi na wafuasi wa chama hicho kumchagua Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Kasimu Amali Makubel pamoja na madiwani wote wa kata 27 Ili kuweza kuwaletea maendeleo.
Aidha katika mkutano huo amewashukuru Wananchi Kwa kuhudhuria mkutano huo Kwa lengo la kusikiliza sera za chama Cha mapinduzi nakuwataka Wananchi wapime hoja za wagombea kisha wafanye maamuzi sahihi ya kuchagua na kupiga kura za ndio Oktoba 29/2025.
Amesema endapo Wananchi mtafanya maamuzi sahihi ya kumchagua rais Dkt Samia Suluhu Hassani na Mbunge,Diwani basi tutahamikisha huduma za Afya zinapatikana Bure hususan magonjwa ya Saratani,Bure na Figo magonjwa atatibiwa Bure.
"Ndugu zangu Wananchi wa Jimbo la Tanga Mjini tunapata ujasili Kila baada ya miaka mitano tunakuja kusimamia jukwaani kuomba ridha ya kuchaguliwa tena Kwa sababu ya Irani ya miaka mitano tuliahidi na tumetekeleza na bado hatuoni chama kingine kitakachofanya vizuri, hivyo ndio maana tumekuja kuomba Watanzania watupe nafasi nyingine ya kwatumikia ikiwemo wanatanga"Alisema Rajabu.
Hodi Wanatanga wenzangu tumekuja na mkataba,Irani ya chama Cha mapinduzi lazima tuwaambie mtuchague chama chetu kimetimiza ahadi mbalimbali za miradi ya maendeleo hivyo tunatembea kufua mbele na kuja kuwaomba tena mtuchague Ili tukamilishe miradi iliyobakia.
"Wanatanga rais Samia Suluhu Hassan yeye kama mgombea anapaswa kutembea kifua mbele Kwa sababu ametekeleza Irani ya chama Tawala Kwa asilimia 100 ndio maana anatembea kifua mbele na kueleza aliyoyafanya katika Mika mitano ya utawala wake madarakani .
Kwa upande wake mgombea kiti Cha Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Kassimu Amali Makubeli amesema irani Bora vipaumbele na tija nataka wanatanga wafahamu kwamba 2030 miradi mingi ya maendeleo ambayo imo ndani ya Irani ya chama Tawala itatekelezwa Kwa asilimia 100
Makubeli ameomba Wananchi wasifanye makosa kuchagua chama kingine Bali nichagueni Ili niweze kuwaletea maendeleo Oktoba 29 mwaka huu tunatia tiki kura zote za ndio Kwa rais wetu na Diwani pia.
"Nitatekeleza vipaumbele vilivyopo ndani ya Irani ya chama Tawala ya mwaka 2025_2030 "Alisema Makubeli.
Alisema Irani ya chama tayari inavipaumbele tayari ambavyo ni ofisi 6 za kata uboreshwaji wa Zahanati nne ambazo,Mawarongo,MapojoniMabokweni ikiwemo ujenzi wa nyumba 13 za watumishi idara ya afya na ujenzi wa jengo la huduma za dhalura



Comments
Post a Comment