DKT. NCHIMBI ATUA MWANGA,AWASHUKURU NA KUOMBA KURA KWA WANANCHI.


Na Ashrack Miraji 

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John  Nchimbi, amewasili Wilayani Mwanga na kuwahutubia Wananchi wa Mwanga kwenye mkutano wake mdogo wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya mikutano vya Cleopa Msuya, leo Jumapili Septemba 14,2025 mkoani Kilimanjaro.

Mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo, Dkt. Nchimbi amepokewa na wazee na viongozi wa kimila wa Jamii ya Wachaga (Mangi) na kumvalisha mavazi ya Kimila na kusimika kuwa mlezi wa Machifu wa Wilaya ya Mwanga.

Baada ya tukio hilo Dkt.Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,aliwahutubia Wananchi hao na baadae  aliitumia nafasi hiyo kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwanga  Ndugu Ngwaru Jumanne Maghembe Ibrahim  pamoja na Madiwani.


Dkt.Nchimbi ambae yuko Kanda ya Kaskazini,anaendelea na miikutano yake ya Kampeni mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.





 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO