MOWASA YANG'ARA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI, MEI MOSI MKOANI KILIMANJARO
MOWASA YANG'ARA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI, MEI MOSI MKOANI KILIMANJARO
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi (MOWASA) imeendelea kung’ara katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi mkoani Kilimanjaro, kwa mwaka huu 2025. MOWASA walitumbuiza kwa uimbaji wa nyimbo iliyoibua shangwe kutoka kwa mamia ya wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro waliohudhuria maadhimisho hayo.
Kabla ya hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyekuwa mgeni rasmi, aliipongeza MOWASA kwa ubunifu wao katika kutoa burudani na elimu ya matumizi sahihi ya maji kwa wananchi. Taasisi hiyo imeonesha mfano bora wa jinsi taasisi za umma zinavyoweza kuelimisha na kuwahamasisha wananchi kwa njia ya ubunifu na ushirikishwaji.
Kwa mwaka huu 2025, maadhimisho ya kitaifa ya Mei Mosi yamefanyika mkoani Singida huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.



Comments
Post a Comment