DKT ABBAS AFUNGUA MAFUNZO KUHUSU ELIMU YA UTALII WA ANGA KWA WADAU WA UTALII
Kassim Nyaki, Karatu.19 Septemba, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amefungua mafunzo ya siku tatu kuhusu elimu ya utalii wa anga (astrotourism) yaliyoanza leo tarehe 19 Septemba, 2025 Karatu Mkoani Arusha.
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) yanatolewa na wataalamu wabobezi kutoka taasisi za Astrotourism Aotearoa (AAA) kutoka nchini New Zealand, Smithsonian Astrophysical Observatory (SAO) ya Chuo Kikuu cha Harvard pamoja na taasisi ya kimataifa ya Dark Sky International yenye Makao Makuu Jijini Arizona, Marekani.
Akifungua mafunzo hayo Dkt. Abbas amesema utoaji wa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Wizara ya Maliasili na utalii kufungua mazao mapya utalii ikiwepo utalii wa Anga ambapo hatua ya sasa ni kutoa mafunzo, maarifa na ujuzi kwa watanzania kuhusu utalii wa anga, vifaa vinavyotumika na fursa zilizopo katika aina hiyo ya utalii.
Prof. John Hearnshaw kutoka New Zeland ambaye ni mwezeshaji wa mafunzo hayo ameeleza kuwa mafunzo yatajikita katika maeneo manne ambayo ni namna ya kuendesha utalii wa anga kwa kushirikisha wadau wa utalii na Jamii, utalii wa anga na Fizikia anga, matumizi ya Telescopic pamoja na upigaji wa picha za utalii wa anga.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na washiriki zaidi ya 70, ambao ni wasafirishaji watalii (Tour Operators), waongoza watalii (tour guides), waendeshaji wa huduma za malazi (Hoteliers ), taasisi za serikali zinazohusika na kutangaza utalii (TTB na ZCT), taasisi za uhifadhi (NCAA, TANAPA, TAWA, na TFS), taasisi za elimu, mafunzo na utafiti (NCT, ACWM-Mweka, VETA, na OUT), Wataalamu wa Utalii, Wasimamizi wa Utalii, Watafiti, Waandaaji wa sera na wafanya maamuzi, Wana-astronomia, Wanafunzi, Wajasiriamali, na watunga sera
Comments
Post a Comment