BALOZI MWAMWETA AMTAKA MWANARIADHA GABRIEL GEAY NA WENZAKE KUIIWAKILISHA VYEMA TANZANIA JIJINI BERLIN



Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassani Mwamweta amewataka wanariadha wanaoshiriki mashindano ya BMW Berlin-Marathon @berlinmarathon-mwaka 2025 kutetea heshima ya nchi kwa kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri katika mashindano hayo, yatakayofanyika Berlin Septemba 21, 2025.

Balozi Mwamweta alitoa kauli hiyo alipokutana na wanariadha hao, wakiongozwa na Bw. Gabriel Geay @gabrielgeraldgeay ofisini kwake jijini Berlin Septemba 19, 2025.

Balozi Mwamweta alisema mashindano ya BMW Berlin-Marathon ni miongoni mwa mashindano makubwa ya riadha Duniani  ambayo mwaka huu yatajumuisha washiriki elfu themanini kutoka duniani kote, hivyo, ushindi wa aina yotote utailetea heshima na kuitangaza nchi ya Tanzania ulimwenguni.

Balozi Mwamweta amewatakia heri wakimbiaji hao katika mashindano hayo na kuwaahidi kuwapa ushirikiano unaohitajika ili waweze kuwakilisha vyema bendera ya Taifa. #BerlinMarathon




Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO