NGORONGORO YAENDELEA KUTOA TABASAMU KWA WAGENI WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA.*



Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) wameendelea kutoa huduma kwa wageni wanaotembelea hifadhi hiyo kwa kuwapa elimu ya vivutio vya utalii, huduma zinazopatikana ndani ya hifadhi, fursa za uwekezaji huku wageni wakionekana kufurahia Wanyama mbalimbali katika mazingira asilia yaliyohifadhiwa.

Wageni na Wananchi wanaotembelea hifadhi ya Ngoromgoro katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja  wanakutana na viongozi na watumishi wa taasisi hiyo kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali katika hifadhi hiyo.

Kauli mbiu ya Wiki ya huduma kwa mteja mwaka huu ni "Dhamira inayowezekana"





Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO