RC BATILDA AWAONYA WAFANYABIASHARA WAKWEPA KODI



Na Boniface Gideon,TANGA

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga imekabidhi Mifuko ya sukari 433 pamoja na madumu 48 ya mafuta ya kula vyote vikiwa na thamani ya Sh. mil.63,255,000, 

Makibidhiano hayo yamefanywa jana na kaimu meneja wa TRA mkoa wa Tanga, Gelas Kinabo pamoja na mkuu wa kituo cha HoroHoro OSBP Shedrack Mbonea   katika kituo cha forodha cha Horohoro  OSBP kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt.Batilda Burian ,ambapo Batilda aliwaonya vikali Wafanyabiashara wanakwepa kodi kwakupitisha bidhaa kwanjia za Magendo. 

Akizungumza katika makibidhiano hayo, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian ametoa shukrani zake za dhati kwa  Mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Tanga kwa kazi kubwa wanayoifanya ambayo imeonekana kwa mapato ya nchi kuongezeka kwa kiwango kikubwa hali inayoonesha kwamba kuna ukuaji wa ulipaji wa kodi kwa hiari bila shuruti,


"tunawashukuru sana TRA,kwa msaada huu,ninawaahidi kuwa utawafikia walengwa,lakini pia niwaombe msiache kuendelea kuisaidia jamii,lakini pia niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya,mnafanya kazi kubwa ambayo imesaidia Mkoa wa Tanga kutoa mchango mkubwa katika Taifa katika sekta ya mapato,tunaomba msibweteke ,fanyeni kazi kwa weledi"Alisisitiza Rc Batilda 

Dkt.Batilda aliwataka wananchi kutumia njia halali za kuingiza mizigo katika mipaka yetu ili kuepukana na  adhabu na kuendelea kufuata sheria mbali mbali za ukusanyaji mapato,

"Niwasihi Wananchi ,hususani wafanyabiashara,wazingatie sheria na kufuata njia sahihi za Biashara,haipendezi hata kidogo kuona mfanyabiashara anataifishwa bidhaa zake kwasababu ya kukwepa kulipa kodi ,mtu anaingiza bidhaa kwa njia za magendo,hii haifai na hakuna mtu atakayefumbiwa macho" Alisisitiza Dkt.Batilda

Kwaupande wake ,Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga  Gelas Kinabo alisema bidhaa hizo ni sehemu ya mali zilizotaifishwa kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu wanaingiza bidhaa kimagendo na kuwataka  wafanyabiashara kufuata taratibu husika za kiforodha wanapoingiza mizigo nchini ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza na kuwataka kuendelea kulipa kodi kwa hiari,

"Bidhaa hizi ni miongoni mwa bidhaa tulizozitaifisha kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu wanaopitisha bidhaa kimagendo,niwaombe wafanyabishara wote ,wafuate taratibu za kiforodha kulipa kodi,wakifuata taratibu za kiforodha hakutakuwa na usumbufu wowote kwa mfanyabiashara"Alisisitiza Kinabo
              

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO