WANANCHI KATA YA KAKESIO NGORONGORO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI*



Wananchi wa kata ya Kakesio iliyoko Tarafa ya Ngorongoro Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha watanufaika na mradi wa Maji kwa ajili ya Mifugo na matumizi ya binadamu kufuatia Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuchimba Kisima cha Maji chenye urefu wa mita 110 ambacho kinatarajiwa kuzalisha maji lita 80,000 kwa siku.                                                                

Uchimbaji wa Kisima hicho ni muendelezo wa kazi nzuri inayofanya na Serikali kwa Wananchi wanaoishi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambapo Kisima kama hicho  kimechimbwa eneo la Mlima matiti kwa ajili ya wananchi wa Kata ya Endulen na Alaetoli na baadae mradi kama huo utatekelezwa katika Kata ya Olbalbal ili kusaidia wananchi kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji kwa mifugo katika msimu wote wa mwaka.



Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO