WAZIRI KOMBO AKUTANA NA BALOZI WA KENYA INCHINI TANZANIA ISAAC NJENGA



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Isaac Njenga, katika jitihada za kuendelea kuimarisha ushirikiano na kuleta maendeleo kati ya nchi hizo mbili.

Wakati wa mazungumzo yao, Waziri Kombo amesisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania kuendeleza uhusiano wa muda mrefu na Kenya, hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji, miundombinu na nishati, ili kukuza uchumi wa pamoja na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Balozi wa Kenya Mhe. Njenga amepongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya mataifa haya mawili jirani na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta za kipaumbele zinazochangia ustawi wa wananchi wa pande zote mbili.




Comments

Popular posts from this blog

HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA WATALII UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

NMB Same Yachochea Ari ya Mafanikio kwa Wanafunzi, Yasema “Bidii, Nidhamu na Malengo” Ndio Siri ya Ushindi

ANNE KILANGO AZINDUA KAMPENI SAME MASHARIKI KWA KISHINDO