SEKTA YA MADINI YACHANGIA UJENZI UWANJA WA MPIRA CHUNYA*



*Ujenzi wafikia asilimia 85*

*Una viwango vya kutumiwa na Timu zote ikiwemo Simba, Yanga, Azam na nyingine*

Chunya

Katika mwendelezo wa kuchangia ukuaji wa  sekta nyingine  kwa maendeleo ya  Taifa na Jamii, shughuli za madini katika Mkoa wa Kimadini Chunya zimechangia ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Kisasa Wilayani humo kupitia michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wa Madini chini ya usimamizi ya Halmashauri husika.

Akizungumza katika mahojiano maalum na timu ya Madini Diary kutoka Wizara ya  Madini,  Mjumbe wa  Kamati ya maandalizi ya ujenzi wa uwanja  huo ambaye pia ni  Mkurugenzi  wa  KenGold Sports Club Keneth Mwakyusa amesema  kuwa, kujengwa kwa uwanja huo kunatokana na jitihada  zilizofanywa na  Halmashauri ya Chunya  kwa kushirikiana na wadau  mbalimbali wakiwemo wa  Sekta ya Madini zilizowezesha kujengwa kwa uwanja huo wa kisasa wa mpira wa miguu.

‘’ Tunaweza kusema mapato ya madini pia yamehusika katika ujenzi wa uwanja kwasababu wadau  waliochangia wapo pia wa madini  ambao  wametumia fedha zilizotokana na  na shughuli za madini lakini wapo na wadau wengine nje ya madini   na usimamizi  mkuu   umefanywa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya akisaidiana na kamati ya ujenzi,’’ amesema.


Ameongeza kwamba, mbali na uwanja huo kutegemewa kutumiwa na timu za Chunya ikiwemo KenGold unatazamiwa katika siku usoni   kutumiwa  kubwa kama Yanga,  Simba, Azam na nyingine  huku  uwepo wake  ukitarajiwa kuchochea ukuaji wa sekta nyingine  kama hoteli, usafiri, chakula na nyingine na kuongeza kwamba hatua iliyofikiwa hivi sasa ni uwekaji wa nyasi bandia.

Akizungumzia mwenendo wa timu ya Kengold amsema kwamba timu hiyo bado inaendelea na mazoezi  na  wana Imani  kwamba itapanda tena daraja na hivyo kutumia fursa hiyo kuwataka wadau wa michezo nchini wakiwemo wananchi wa Chunya kuendelea kuiunga mkono timu hiyo.

‘’Timu  yetu ipo inaendelea na mazoezi, kwa mfano hivi karibuni ilicheza mchezo wa kirafiki na Songwe na zote zilitoka suluhu ya  mabao mawili kwa  mawili 2-2 kwa hivyo bado tuna imani  ya kurejea ligi Kuu,’’ amesisistiza,’’.

Naye, Fundi wa uwanja huo Msafiri Napanja amesema kazi inayoendelea  hivi sasa ni uwekaji wa nyasi bandia iliyopangwa kufanyika ndani ya siku 30 huku maendeleo ya ujenzi wa uwanja yamefikia asilimia 85.

Awali, akizungumza na timu hiyo ya Madini Diary, Afisa Madini Mkoa wa Kimadini Chunya Mhandisi Laurent Mayalla amesema kwamba mchango wa Sekta ya madini wilayani chunya umeyagusa maeneo mengi ikiwemo ya michezo kutokana na ujenzi wa uwanja  huo.

 *#Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri



Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO