KATIBU MKUU WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA



Geita, Septemba 22, 2025

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita.

Katika ziara hiyo, Mhandisi Samamba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo pamoja na viongozi waandamizi wa Tume ya Madini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume, Dkt. Janet Lekashingo, pamoja na Makamishna wa Tume, Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi.

Ziara hiyo imelenga kukagua na kujionea ubunifu na teknolojia mbalimbali zinazotumika katika sekta ya madini, huku Tume ya Madini ikiendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu fursa na wajibu wao katika maendeleo ya sekta hiyo.




Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO