SIMBU AMBAYE NI BINGWA WA MBIO ZA DUNIA AWASILI NCHINI
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha, ameongoza mapokezi ya Mwanariadha Sajini Alphonce Simbu ambaye ni Bingwa wa mbio za Dunia kwa Wanaume na mshindi wa Medali ya Dhahabu, aliyewasili nchini alfajiri ya Septemba 23, 2025 akitokea Tokyo Japan alikoshiriki mbio hizo.
Mapokezi hayo pia yamehudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) pamoja na familia yake.
Comments
Post a Comment