WANANCHI WA TANGA WAJIANDAA KUPOKEA MGOMBEA URAIS SAMIA SULUHU HASSAN SEPTEMBER 27
Na, Agnes Mambo,Tanga.
MGOMBEA URAIS na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassani anatarajia kuwasili Mkoani Tanga Septemba 27 atapokelewa Mkata,Handeni,kisha Septemba 29 na 30 atafanya mikutano ya hadhara Kwa Wananchi kunadi sera za chama chake.
Akitoa Taarifa Kwa vyombo vya habari Mkoani Tanga,MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdulrhaman amesema kwamba mgombea Urais wa Chama hicho Dkt. Samia Suluhu ni kiongozi aliyejipambanua kuwaletea watanzania maendeleo kutokana na kasi ya utendaji wake.
Rajabu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (MCC) aliyasema hayo Septemba 22 majira ya saa nane mchana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo kuhusu ujio wa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Samia Suluhu Hassani
Mwenyekiti Rajabu amesema Mgombea URAIS Dkt Samia Suluhu Hassani atafanya kampeni zake Kwa siku tatu mfululizo na atakwenda pia maeneo maalum aliyopangiwa kwenda kuzungumzia na Wananchi ikiwemo,MUHEZA,Korogwe pamoja na maeneo mengine kunadi sera za chama hicho Ili kupata ridhaa ya kuwaongoza wanatanga na Watanzania Kwa ujumla.
Alisema kwamba Dkt Samia atapokelewa Mkata wilayani Handeni baada ya hapo atapumzika jijini Tanga na siku inayofuata Septemba 28 ataanzia wilaya ya Pangani kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara wilayani humo.
Alisema kwamba anayokuja kuwahutubia kupitia ilani ya uchaguzi 2025/2030 baada ya kuunda Serikali maendeleo yatakayokuja kwa ajili ya wananchi wote hiyo niwaombe wana CCM wote popote walipoo kila mmoja wanawakaribisha kujitokeza kumlaki mgombea huyo.
“Niwaombe wananchi na wana CCM na vyama vingine vya upinzani wote kila mmoja tunawakaribisha kumlaki na kumpokea Mgombea wa Urais kupitia CCM hatuna mgombea mwengine zaidi ya Dkt Samia tujitokeza kwa wingi na baada ya kumalizia Mkutano Tanga mjini atapita Muheza, Korogwe na ratiba katika maeneo hayo zitatolewa kwa nyakati tofauti”Alisema Mwenyekiti huyo.
Amesema wana Tanga wanajiona watu wenye bahati kupata ugeni huo mkubwa kwa mara ya pili kwa mwaka huu mmoja amekuja kwa ziara ya kikazi miezi michache iliyopita mwaka huu na alikpokuja Tanga mambo mengi ya kimaendeleo ya Tanga yamefunguka na mambo yalikwenda vizuri na sasa anakuja kama Mgombea Urais.
Mwenyekiti wa CCM mkoa amesema wananchi wa mkoa wa Tanga wanategemea maendeleo zaidi kwa sababu kuna utofauti kati ya Mgombea wa CCM na wengine kutokana na kwamba wao walihaidi na wameshafanya kupitia ilani ya uchaguzi na aliyekuwa mtekelezaji ni Rais Dkt Samia Suluhu.
Alisema kwamba kutokana na mambo makubwa ya kimaendeleo yaliyokwisha kufanyika imani yao ni kwamba wananchi watakiunga mkono chama chao kwa sababu wana imani kwamba wakihaidi wanatekeleza kwa vitendo.
"Tunamatumaini makubwa watu watampa kura nyingi Rais Dkt Samia Suluhu kwa sababu namna alivyojipambanua katika suala la kulinda amani ya nchi kwa kutumia busara na hekima na miradi mikubwa ya maendeleo"Alisema Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga.
Dkt Samia alipokuja katika ziara ya kikazi kabla ya kuja kuna miradi ilikuwa inasuasua lakini baada ya kuja,miradi imefunguka mfano barabara ya Tanga-Sadani -Bagamoto kasi ilivyoongezeka na Barabara ya Soni –Bumbuli mpaka Dindira na Korogwe kupitia kwa Meta wameona barabara hiyo wataalamu wanakwenda kuanza muda msio mrefu.
Aliongeza kwamba hiyo yote ni baada ya ujio wake hivyo wanaamini anapokuja anakwenda kuwaidi yale yaliyopo kwenye ilani mpya ya uchaguzi na miradi iliyobaki itakwenda kutiliwa mkazo itamalizika na miradi mipya iweze kuanzishwa .
Comments
Post a Comment