KIGIDA CHAOKOA AFYA NA MAZINGIRA KATIKA UCHENJUAJI DHAHABU


Geita, Septemba 25, 2025

Tume ya Madini imeendelea kutoa elimu kwa wachimbaji kuhusu matumizi ya Kigida (Retort), kifaa kinachosaidia kulinda afya za wachimbaji, mazingira na kupunguza gharama za matumizi ya zebaki katika uchenjuaji wa dhahabu.

Akizungumza kwenye Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita, Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Hyasinta Rugeiyamu, amesema Kigida kimeundwa kwa mfumo unaozuia mvuke wa zebaki kuingia mwilini wakati wa uchenjuaji, hivyo kumlinda mchenjuaji dhidi ya madhara ya kiafya.

“Mbali na kulinda afya, Kigida huzuia pia moshi wa zebaki kutawanyika hewani. Badala yake, mvuke huo hubadilishwa kuwa kimiminika kinachohifadhiwa na kutumika tena. Hii husaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na gharama za ununuzi wa zebaki mpya,” amefafanua Rugeiyamu.

Ameongeza kuwa Tume ya Madini itaendelea kuhamasisha wachimbaji kote nchini kutumia Kigida ili kuhakikisha shughuli za uchenjuaji zinafanyika kwa usalama, tija na uendelevu.






 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO