REA KIVUTIO KIKUBWA UUZAJI WA MAJIKO BANIFU KWA BEI YA RUZUKU*
*📌Banda la REA limepamba Maonesho ya Madini Geita*
*📌Majiko ya gesi ya kupikia nayo yanatolewa kwa bei ya ruzuku Geita*
📍Geita
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kuuza majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita.
Katika maonesho ya madini, REA inauza majiko banifu kwa gharama ya shilingi 6,200 tu ambapo kabla ya ruzuku kutolewa na Serikali majiko hayo yaliuzwa kwa gharama ya shilingi 41,300.
Majiko banifu yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kupunguza sumu ya mkaa (carbon monoxide) hivyo kusaidia kupunguza madhara ya kiafya yatokanayo na nishati ya mkaa.
Katika mkoa wa Geita kampuni inayosambaza majiko banifu kwa bei ya ruzuku ni Geita Millenium Star Company Limited.
Comments
Post a Comment