KILA JIWE LINA THAMANI – KERAKA


Geita

MJIOLOJIA kutoka Ofisi ya  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara, Godfrey Keraka, amesema kuwa kila jiwe lina thamani kwa sababu ya mchango wake katika sekta ya madini, maendeleo ya taifa na teknolojia ya kisasa duniani.

Akizungumza kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Keraka ameeleza kuwa sekta ya madini inachangia  asilimia 10.1 ya Pato la Taifa (GDP) na ni urithi muhimu wa nchi unaopaswa kulindwa.

Ametolea mfano wa madini ya vito kama Amethyst, Rose-Quartz na Quartz ambayo hutumika kutengeneza mapambo ya thamani, wakati madini ya chuma yanahusishwa zaidi na ujenzi wa miundombinu, utengenezaji wa magari, meli na mashine mbalimbali. Aidha, shaba hutumika kwenye nyaya za umeme, feldspar kwenye vigae na mapambo, na pyrite kwenye mbolea, mapambo pamoja na uzalishaji wa tindikali ya salfyuriki.

Kwa upande mwingine, makaa ya mawe yametajwa kuwa chanzo muhimu cha nishati, huku dhahabu na fedha zikibainishwa kama madini yenye thamani kubwa yanayotumika katika hifadhi ya fedha, mapambo, sarafu na vifaa vya kielektroniki. 


Keraka pia amesisitiza umuhimu wa graphite na lithium kama madini ya kimkakati katika utengenezaji wa betri na mifumo ya kuhifadhi nishati.

“Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa kila jiwe lina thamani kubwa. Miamba na madini ni urithi wa taifa unaopaswa kulindwa na kutumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho,” amesema Keraka.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO