TARURA KUPITIA DARAJA LA MAWE MAJIMOTO KUKUZA SEKTA YA KILIMO, MPIMBWE-KATAVI*


📌Mradi wote wafikia  95% ya utekelezaji

 Mpimbwe, Katavi

Ujenzi wa Daraja la mawe katika mto Katupa sambamba na ujenzi wa barabara ya Majimoto-Namanyele inayojengwa kiwango cha changarawe katika Halmashauri ya Mpimbwe Mkoani Katavi umetajwa kukuza sekta ya kilimo na kuboresha uchumi wa Wakulima.

Meneja wa Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Mlele Mhandisi Paul Mabaya, amesema thamani ya ujenzi wa mradi huo ni shilingi 361,950,000.00 ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 95. 

Mhandisi Mabaya amesema mradi huo pia unajumuisha ujenzi wa Daraja la mawe, barabara ya kiwango cha changarawe kilomita 1.5 na ujenzi wa kalvati tatu huku fedha za utekelezaji wa mradi huo ni sehemu za fedha za ufadhili kutoka Benki ya Dunia kupitia mradi wa  "RISE" 

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa  mwaka 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuchochea maendeleo yao. 

Naye Mkazi wa kijiji cha Majimoto Shija Shigela, licha ya kuishukuru TARURA kwa ujenzi wa mradi huo pia ameiomba kuendelea kujenga miradi mingi zaidi ya barabara nchini.



 

Comments

Popular posts from this blog

HATMA YA TAIFA IPO KATIKA USAWA WA KIJINSIA, SIO VIWANDA PEKEE.

MSAKO MKALI KUREJESHA HALI ya USALAMA TANGA, WATUHUMIWA 42 WAKAMATWA

PJT-MMMAM YAWEZESHA UANZISHWAJI WA VITUO 206 VYA MALEZI YA WATOTO WADOGO